Na Wanderi wa Kamau
NAKURU MIAKA MITATU BAADA YA MACHAFUKO YA 2007/2008
Wakati Kenya ilipowaka moto mnamo 2007 baada ya kutangazwa kwa matokeo ya uchaguzi tata wa urais,maeneo mengi ya nchi,Nakuru ikiwemo,yalibadilika.Jamii nyingi ziligeukiana zenyewe kwa misingi ya tofauti za kisiasa.Taharuki ya kisiasa iliyotanda kotekote ililipuka na kuwa uporaji, ubakaji na hata mauaji.
Maelfu ya watu walifurushwa kutoka makwao.Huku haya yakijiri,kaunti ya Nakuru haikusazwa.Aghalabu Nakuru ilikuwa mojawapo ya sehemu zilizoathiriwa zaidi na machafuko haya.Kijografia,Nakuru ni makao kwa wakaazi wengi wanaotoka sehemu mbalimbali za Kenya.Miongoni mwa jamii zinazoishi katika kaunti hii ni kama Wakikuyu,Wakalenjin,Wakamba,
Wakisii,Waluo miongoni mwa jamii nyingine.
Aidha jamii hizi huwa na tofauti nyingi za kitamaduni,kimitindo na hata kisiasa.Hivyo basi,utata wa uchaguzi wa 2007,ulileta tofauti nyingi tu miongoni mwa wakaazi hawa ambazo zililipuka na kuwa vita vya kikabila.
Lakini miaka mitatu baadaye,eneo hili ni tofauti sana.Kwa mijibu wa uchunguzi wetu,jumbe za kuhubiri amani na picha za athari za machafuko haya ya kikabila,zimejaa kila mahali.Kwa mfano,katika mtaa wa Kaptembwa,mojawapo wa mitaa iliyoathirika zaidi na vita hivi,jumbe hizi zimewekwa katika maduka,mahoteli na hata vituo vya burudani ili kuwakumbusha wakaazi wa hapa kila kuchao,madhara yanayofungamana na machafuko ya kikabila.
Kulingana na John Njoroge,mkaazi wa mtaa huu aliyechomewa maduka yake mawili,hali ni tulivu kwa sasa."Tulipiga kura kwa amani wakati wa kura ya maoni mnamo Agosti,4 ,2010.Hakuna lililotokea au taharuki iliyotanda baadda ya matokeo ya kura kutangazwa,"anasema Njoroge.
Juhudi za kuzipatanisha jamii mbalimbali katika kaunti ya Nakuru na mkoa wa Bonde la Ufa kwa jumla zimeonekana kuzaa matunda,miaka mitatu baadaye,kwa mujibu wa diwani Joel Gitimu wa wadi ya Lenginet,aliye pia mwanachama wa kamati ya amani katika eneo hilo."Yaonekana wakaazi wengi katika kaunti hii walijifunza sana kutokana na athari zilizotokea hapa.Maendeleo yalidumazwa na ustawi wa kiuchumi ilididimia kwa kiwango kikubwa,"anaeleza diwani Gitimu.
Sehemu zingine zilizoathiriwa na machafuko haya ni kama Githima,Rhonda,Marigat,Molo miongoni mwa zingine.
Askofu John Kimani William wa kanisa la Kingdom Seekers,mjini Nakuru na wachungaji wengine vile vile wamekuwa katika mstari wa mbele kuzihamasisha jamii mbaimbali humu nchini kutojiingiza tena katika chuki za kisiasa na kikabila.Aidha askofu huyu amekuwa akizitembelea sehemu mbalimbali humu nchini akiwashajiisha Wakenya kujitenga na chuki ambazo ni kizingiti kikubwa cha maendeleo.
Wasomi vile vile hawajabaki nyuma.Walizikusanya fikra na tajriba zao ili kuweza kuandika makala na vitabu vitakavyowasaidia Wakenya kujifunza kwa undani kuhusu athari za machafuko ya kikabila.Aliyekuwa mbunge wa Subukia, Koigi wa Wamwere katika kitabu chake Kuelekea Mauaji ya Kimbali Nchini Kenya:Laana ya Ukabila Hasi anaonya Wakenya wajifunze na yaliyotokea Rwanda mnamo Aprili 1994 wakati jamii za Wahutu na Watutsi zilijiingiza katika mzozo wa kimamlaka."Umaskini ndicho chanzo cha michafuko hii tangu 1992 wakati mfumo wa vyama vingi ulipoanzishwa,"anasema mwandishi huyu katika utangulizi wa kitabu chake.
Eneo la Nakuru liliathirika vibaya kwa kiwango ambacho serikali ililazimika kuweka amri ya kutotoka nje ili kupunguza taharuki iliyotanda.
Huku duru ya pili ya vikao vya mahakama ya ICC ikitarajiwa kuanza mnamo tarehe 21 Septemba,waathiriwa wa ghasia hizi bado wamo hemani eneo la Pipeline,Nakuru.Wengi wao wamepoteza matumaini na kupata haki.Lakini wanautegemea mchakato wa kusikilizwa ka kesi huko Hague kwamba hatimaye utatenga mbivu na mbichi na haki itapatikana.
"Tunaiomba serikali kututafutia makao mbadala kwani mvua inayoendelea kunyesha ni tishio kubwa kwa afya za watoto wetu,"anaeleza Felistus Wangechi,mmojawapo wa wakimbizi wa ndani kwa ndani wa vita hivi.Kambi hizi ni mojawapo ya makovu ya athari za machafuko haya kando na nyumba zilizochomwa,hasa katika eneo na Githima na Kaptembwa.
Mji wa Nakuru umebadilika na majengo makubwa makubwa ya kibiashara yanaonekana.Vile vile,vyuo vingi vimeanzisha matawi yao mjini hapa-ishara ya kuinuka kwa kiwango cha elimu.

No comments:
Post a Comment